Jumapili, 5 Machi 2017

Zitto kabwe:mkandarasi wa maji amefilisika.

Zikiwa zimepita siku mbili toka Rais Magufuli atoe amri kushikiliwa kwa hati za kusafiria za mwakilishi wa kampuni ya ukandarasi ya Overseas Infranstructure Alliance Private Limited ya India Bw. Rajendra Kumar pamoja na wasaidizi wake.

Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe ameibuka na kusema toka mwaka 2016 amekuwa akiimba na kuimbia Serikali juu ya Mkandarasi wa Mrdai wa Maji Kigoma kuwa amefilisika na hatua zichukuliwe juu yake lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Hivyo basi Mbunge huyo anahoji kwa Wizara ya Maji kuwa inahitaji mpaka Rais Magufuli afike Kigoma ndiyo ichukue hatua dhidi ya Mkandarasi huyo?
"Juzi nimeona Rais anatoa amri kali kuhusu mradi wa Maji wa Lindi. Tangu mwaka 2016 nimekuwa nikiiambia Serikali kuwa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Kigoma amefilisika na hatua zichukuliwe.

 Hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya kampuni ya Spencon. Nilionya kwenye mkutano wa hadhara Bangwe mwezi February mwaka 2016, nikauliza swali Bungeni na kuzungumza Bungeni suala hili mwaka 2016. Mara zote Serikali ilisimama kusema mradi utakwisha Oktoba ama Disemba 2016. Wizara ya Maji inahitaji Rais aje Kigoma ndio ichukue hatua? " alihoji Mhe. Zitto Kabwe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni